Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

MODERN SOFAS FOR SALE






Sofa hizi za kisasa zinauzwa. Ni za brown na zina kitambaa kizuri sana na imara. Seat zake ni za Golden black and brown flowery.


Zipo tatu, moja la watu watatu, moja la watu wawili na moja la mtu mmoja na Sofa stool (seat sita kwa ujumla). Yanaenda kwa Tshs. 1.500,000/= bila majadaliano


mawasiliano piga : +255 713 076878
                             +255 765 222111

PLOT FOR SALE

Eneo linauzwa, lipoMbezi Mpiji  kilomita sita kutoka barabara ya morogoro. 

Size:
Lina ukubwa wa miguu 20X20 na lipo katika planned street. Barabara za mtaa zote zimepimwa. Ni eneo tulivu na lenye usalama.

Price:
Tshs 5,500,000/= (milioni tano na laki tano za kitanzania) 

Directions:
Kutokea ubungo unaenda hadi Mbezi mwisho mkono wa kulia kuna barabara ya vumbi, ina kibao kimeandikwa mpiji magohe na kibao cha Mbezi secondary school. Unachukua hiyo barabara moja kwa moja uningia kilomita sita ndani then kuna centre ya maduka maduka mknono wa kulia kuna duka limeandikwa "Mkuu wa kituo" ukifika hapo piga simu utafuatwa

Contacts:
Simu namba +255 718 303375

IDARA YA UHAMIAJI INACHANGIA WAFANYAKAZI WATANZANIA KUNYONYWA

Hili ni wazo langu tete, 

Katika miaka ya karibuni kumekua na wimbi kubwa la kuongezeka kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini. Nia na madhuni makubwa ya serikali kuruhusu wageni hawa kupewa vibali vya kufanya kazi hapa nchni ilikua ni kuona kwamba ujuzi wao waliokuja nao unafundishwa kwa watanzania ambao hatimae watakua na uwezo wa kufanya kazi hizo zinazofanywa na wageni hao.

Wageni waliokua wanatakiwa kupewa vibali ni watu ambao wana ujuzi wa hali ya juu amabao baadae utakua na faida kwa nchi yetu, na pia nina amini kwamba wageni hawa walikua wana limit ya muda wanaoruhusiwa kukaa nchini, muda ambao utakua umetosha kufundisha watanzania ujuzi ule na kisha kwenda zao kwao.

Sasa basi, sababu zinazonifanya mimi niseme kwamba idara ya uhamiaji inachangia sisi watanzania kunyonywa ni hizi;-

1. Wageni wanaoingia siku hizi wengi wao hawana ujuzi wowote wa ajabu , wengi wao wanaingia na qualifications ambazo watanzania wa kawaida wanazo, tena wengi sana na wapo mtaani hawana kazi. Na wageni hawa wanapofika makazini hupewa huduma zote bure zikiwemo afya, makazi, usafiri, na hadi ada za watoto, zaidi ya hayo wageni hawa wanalipwa kwa dola za kimarekani na mishahara yao yote huanzia dola $1000 hadi $10,000. 

Kwanini idara ya uhamiaji iruhusu kampuni iingize accountant kutoka nje? ilhali kuna graduates hadi wa masters wa mambo hayo hayo ya uhasibu na wako mtaani hawana kazi? 

2. Mishahara wanayolipwa watanzania tena wenye qualifications zinazowazidi hawa wageni inatia huruma, yani unakuta mtanzania mwenye expirience kabisa na elimu yake ya kutosha mshahara wake haufiki Tsh. 900,000/= . na mshahara huu unakuja mkavu bila beneft ya aina yeyote nyingine. Hii ni haki kweli?

3. Na la mwisho na kubwa zaidi ni kwamba wageni hawa HAWAONDOKI! yani kuna wageni ambao permits zao zinakua - renewed kila zinapoisha kwa karibia miaka ishirini sasa. hivi sisi hatujifunzi tu kutoka kwao? yani miaka kumi, ishirini kweli hakuna mtanzania hata mmoja ambae anakua ameweza kumaster kazi hizo zinazofanywa na hawa expatriates? mbaya zaidi ni kwamba watu hawa matumizi yao yote makubwa huenda kuyafanya makwao wanapoenda likizo, hivyo basi watanzania hakuna hata moja tunalofaidika nalo kwa kuwalipa mishahara hii mikubwa.

Hapo bado hatujazungumzia jinsi wanavyowatreat watanzania wanaofanya kazi kwenye taasisi ama viwanda vyao, hii sio haki hata kidogo na jambo hili linatakwa liangaliwe mara moja na kushughulikiwa. 

Taasisi zenye huu mtindo wa  kuajiri hadi wapaka rangi kutoka nje ni pamoja na mashirika yote yasiyo ya kiserekali (NGOs) tena haswa zile za kimataifa mi mi staki kutajana majina. Makampuni yote yanayomilikiwa na watu wenye asili ya kiasia (India na China) ndiyo yanaongoza kw kuajiri watu kutoka nje. Tena nje ya idadi inayoruhusiwa kisheria.

Maswali yangu mimi ni je inakuaje mtu anakaa nchini kwetu kwa miaka kumi na zaidi? 

Kwanini hamna bodi inayoangalia mishahara ya wafanyakazi wote tu kwa ujumla kuhakikisha kwamba watu wenye ujuzi na ufanisi sawa wanalipwa mishahara sawa bila kuangalia utaifa wao? 

Na je inakuaje makampuni yanazidisha idadi ya wageni iliyowekwa na serikali? 

Na mwisho kabisa inakuaje mtu ambae hana ujuzi wowote wa ajabu ambao nchini kwetu haupo anapata kibali cha kufanya kazi nchini?

Swali la mwisho la muhimu kabisa ni kwamba Je mapato yao haya yote yanalipiwa kodi????????? wahusika tafadhalini hebu pitieni hizi ofisi na mashirika mjionee mambo. wachache wanakula na wanafaidi lakini athari wanayowaletea watanzania haielezeki.

Hii ni kwa niaba ya watanzania wote wenye ujuzi ambao mpo mtaani kwa kukosa kazi.

UHURU KENYATTA AJIUZULU KENYA.


Kenyan Finance Minister Uhuru Kenyatta in a file photo. President Mwai Kibaki has accepted the resignation of  Kenyatta, the presidential spokesman said on Thursday.  REUTERS/Thomas Mukoya
- Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Uhuru Kenyatta amejiuzulu leo siku chache baada ya jina lake kuonekana katika watuhumiwa wa uchochezi wa fujo za uchaguzi wa mwaka 2007 iliyotolewa na mahakama ya kimataifaa ya makosa ya jinai (ICC) hivi karibuni.
 Kujiuzulu huko kwa Kenyatta kumeenda sambamba na kiongozi mwingine wa umma bw. Francis Muthaura.
 
 
           Hata hivyo katika kuonesha kuwa huo sio mwisho wa harakati zake katika siasa Kenyatta amehusishwa nu kugombea urais mwaka 2013 safari hii akiungana na aliyekuwa adui yake katika fujo na uchaguzi wa mwaka 2007 ndugu William Ruto ambaye pia ni mtuhumiwa wa ICC katika fujo hizo za uchaguzi wa mwaka 2007. Kenyatta na Ruto wanadaiwa kuchochea makundi ya vijana kutoka katika itikadi, makbila  na sehemu tofauti  kupigana na kuuana punde baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya mnamo mwaka 2007 kumalizika.
 
           Kenyatta mwenye miaka 50 mtoto wa Jomo Kenyatta baba wa taifa la Kenya na tajiri zaidi Nchini Kenya alikuwa akipata shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa wabunge wenzake kufuatia kupatikana na kesi ya kujibu na mahakama ya kimataifa ya makosa ya Jinai.
 
           Ni desturi nchini Kenya kwa mawaziri wanaotuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi za umma kujiuzulu ingawa Mwanasheria mkuu wa Kenya Kenyatta and Muthaura wangeweza kuendelea na nafasi zao mpaka hapo rufaa walizokata kwa mahakama hiyo ya kimataifa kukataliwa suala ambalo huchukua hadi mwaka mmoja.

MZAHA WA VAZI LA TAIFA KUTOKANA NA BENDERA YA TAIFA?

Ni jambo lisilopingika kua kila nchi ina bendera yake, bendera ambayo huwakilisha nchi hiyo katika masula mbalimbali ya kimataifa. kuna symbols nyingi sana ambazo huwakilisha nchi husika, kama nchi. Lakini pia kuna yale mambo ambayo huwakilisha tamaduni na desturi za watu wanaoishi katika hizo nchi.

Ni uelewa wangu kwamba mchakato wa kutafuta vazi la taifa umeanza rasmi, kwa mara nyingine tena.  Vazi hili litakua mahsusi kwaajili ya kutambulisha utamaduni wa mtanzania popote pale duniani. Kamati/Tume iliyoundwa kutengeneza vazi hili imeamua "Kutumia rangi za bendera ya taifa" katika mchakato mzima wa kutengeneza vazi hili. 

Kwa mtazamo wangu huu ni utani usiochekesha. Imagine vazi lenye rangi za njano, kijani,blue na nyeusi??? maswali ya kujiuliza ni kwamba ni nchi ngapi ambazo zinatumia rangi zinazoendana na na za bendera yetu? Na je ni nchi ngapi za kiafrika tunazozijua ambazo kiukweli zina mavazi ya taifa yaliyotokana na bendera ya nchi zao? na je ujumbe ambao vazi la taifa linatakiwa kufikisha utafika kwa kutumia rangi za bendera ya taifa? na mwisho kabisa swali la muhimu ni kwamba msafara wa kitaifa ambao umepembwa na bendera za taifa zinazopepea na zingine zilizovaliwa utaonekanaje?

Suala lilijitokeza hapa ni watu kukosa ubunifu. Samahani kwa nitakaowakwaza lakini mtazamo wangu ni kwamba nchi hii ina makabila mengi sana yenye tamaduni nzuri sana ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kuchangia katika uppatikanaji wa vazi la taifa, zaidi ya hayo nchi ina rasilimali nyingi sana amabazo kitambaa cha vazi la taifa kinaweza kutumika kufikisha ujumbe huo kwa jamii za kimataifa, kuliko kutumia bendera ambayo tayari inajulikana.

Kuazia utamaduni wa shanga za wazaramo, kaniki za wamakonde , rubega za wamasai, shanga za miguu za waha na na makabila mengine yoote yenye mavazi ya asili, tumeshindwa kweli kujumuisha tamaduni hizi na kupata tamaduni moja itakayotuunganisha watanzania wote hadi tunaamua kutumia rangi za bendera?  Mzaha huu, sijauelewa kabisa

Huu ni mtazamo wangu waungwana, msijenge chuki 

ALEK WEK




Born Alek Wek
16 April 1977 (age 34)
Wau, South Sudan 
 Height 5 ft 11 in (1.80 m) 
 Hair color Dark Brown 
 Eye color Brown 
 Measurements 34-23-34.5 (US) 86.5-58-88 
 Dress size 4 (US) 
 Agency Storm Models, London

Alek Wek (born 16 April 1977) is a South Sudanese British model who first appeared on the catwalks at the age of 18 in 1995, sparking a career lasting to date. She is from the Dinka ethnic group in South Sudan,but in 1991 she and some family members fled to Britain to escape the civil war in Sudan. She later moved to the United States. 
 
   



  

She was born the seventh of nine children in Wau in Sudan (now South Sudan) in 1977. When she was preparing to emigrate from Sudan, her mother picked the date April 16, which occurs in the rainy season during which she was born. She says her name means "Black Spotted Cow". Wek was born to her mother  a housewife, and her father Athian Wek (1933-1985), an education official. Alek Wek has stated that physically, she resembles her father, who also had unusually long limbs. Athian Wek had once broken his hip in a bicycle accident; his hip was repaired with metal pins. When the civil war broke out in Wau in 1985, the Wek family had to flee from both rebel and government forces. Long periods of walking caused Athian Wek's hip to get infected, and upon the family's return to Wau, he became paralyzed and endured a hemorrhage. He died in the hospital of Khartoum.




Wek was discovered at an outdoor market in London in 1995 in Crystal Palace, south London, by a Models 1 scout. She first received attention when she appeared in the music video for "GoldenEye" by Tina Turner, in 1995 and from there entered the world of fashion as one of its top models. She was signed to Ford Models in 1996 and was also seen in the "Got 'Til It's Gone" music video by Janet Jackson that year. She was named "Model of the Year" in 1997 by MTV. She was the first African model to appear on the cover of Elle, also in 1997.




She is a member of the U.S. Committee for Refugees' Advisory Council and is helping to raise awareness about the situation in Sudan, as well as the plight of refugees worldwide. She can base this on her own experience as a refugee, fleeing the war in her country of birth.She is a missionary for World Vision, an organisation which combats AIDS, an ambassador for Doctors Without Borders in Sudan, and devotes time to. In 2007, she released an autobiography, entitled Alek: From Sudanese Refugee to International Supermodel, documenting her journey from a childhood of poverty in Sudan to the catwalks of Europe































Nominees in main Oscars categories



Best picture: "War Horse," "The Artist," "Money Ball," "The Descendants," "The Tree of Life," "Midnight in Paris," "The Help," "Hugo," "Extremely Loud and Incredibly Close."

- Best director: Michael Hazanavicius for "The Artist,"
Alexander Payne for "The Descendants,"
Terrence Malick for "The Tree of Life,"
Woody Allen for "Midnight in Paris,"
Martin Scorsese for "Hugo."

- Best leading actor: Demian Bichir in "A Better Life,"
George Clooney in "The Descendants,"
Jean Dujardin in "The Artist,"
Gary Oldman in "Tinker Tailor Soldier Spy,"
Brad Pitt in "Moneyball"

- Best leading actress: Glenn Close in "Albert Nobbs,"
Viola Davis in "The Help,"
Rooney Mara in "The Girl with the Dragon Tattoo,"
Meryl Streep in "The Iron Lady,"
Michelle Williams in "My Week with Marilyn."

- Best supporting actor: Kenneth Branagh in "My Week with Marilyn," Jonah Hillin "Moneyball,"
Nick Nolte in "Warrior,"
Christopher Plummer in "Beginners,"
Max von Sydow in "Extremely Loud & Incredibly Close."

- Best supporting actress: Bérénice Bejo in "The Artist,"
Jessica Chastain in "The Help,"
Melissa McCarthy in "Bridesmaids,"
Janet McTeer in "Albert Nobbs,"
Octavia Spencer in "The Help."

- Best foreign language film: "Bullhead" (Belgium), "Footnote" (Israel), "In Darkness" (Poland), "Monsieur Lazhar" (Canada), "A Separation" (Iran).
- Best animated feature: "A Cat in Paris," "Chico & Rita," "Kung Fu Panda 2," "Puss in Boots," "Rango."



GOOD LAUGH - MARRIAGE PROPOSAL IN PUNJABI ENGLISH

Madam :
 I am an older young uncle living
 only with myself in Lahore . Having seen your advertisement
for marriage purposes, I decided to press myself on you and
 hope you will take me nicely and easily.

 I am a soiled son from inside Punjab . I am nice and big,
 six foot tall, and six inches long. My body is filled with
 hardness, as because I am working hardly. I am playing
 hardly also. Especially I like cricket, and I am a good
batter and I am a fast baller. Whenever I come running in
 for balling, other batters start running. Everybody is
 scared of my balls because they bounce a
 lot.

 I am very nice man. I am always laughing loudly at
 everyone. I am happy and I am
 gay. ladies, they are saying I am nice and soft. Am always
 giving respect to the ladies. I am always allowing ladies to
 get on top. That is how nice I am. I am not having any bad
 habits. I am not drinking and I am not sucking cigarettes
 or anything
 else. Every morning I am going to the Jim and I am pumping
like anything. Daily I am pumping and pumping. If you want
 you can come and see how much I am pumping the dumb
 bells in the Jim.

 I am having a lot of money in my pants and my pants is
 always open for you. I am such a nice man, but still I am
 living with myself only. What to do ? So I am taking things
 into my own hands everyday... That is why I am pressing
 myself on you, so that you will come in my house and
 take my things into your
 hands.

 If you are marrying me madam, I am telling you, I will be
 loving you very hard every day.. fact, I will stop pumping
 dumb belles in the Jim. If you are not marrying me madam and
 not coming to me, I will press you and press you until you
 come. So I am placing my head between your nicely smelling
 feet looking up with lots of hope.

 I am waiting very badly for your reply and I am stiff with
 anticipation.

 Expecting soon

 Yours and only yours

 Choudhary Warraich,------------------
 born by mother in Okara
 and become big in Lahore ,
 Punjab

MBUNGE MWINGINE AFARIKI DUNIA


TAARIFA ya iliyotufikia hivi punde katika inaeleza kuwa mbunge wa jimbo la ARUMERU kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mh. Jeremia Sumari (pichani) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mh. Jeremia Sumari ni Mbunge wa pili kufariki dunia kwa mwaka huu 2012 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutanguliwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Morogoro,Marehemu Regia Mtema aliyezikwa nyumbani kwao Ifakara Mkoani Morogoro jana na mazishi yake yaliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Kikwete.

Blogu hii inaendelea kufuatilia taratibu zote za msiba huu na tutaendelea kutoa taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Mungu ailaze roho za marehemu mahala pema peponi

-Amen


source: http://mrokim.blogspot.com/2012/01/mbunge-mwingine-afariki-dunia-leoni.html

KISARAWE LUTHERAN JUNIOR SEMINARY 20YEARS ANNIVERSARY

Wapendwa,

Kwa wale wote mliopita katika shule hii, kwa namna moja au nyingine hapa mahali pamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuwa watu tulio leo. Hii shule ilianzishwa kwa nguvu za walutheran wa Tanzania, na mimi kama mmoja wa watu waliopita hapa, nakubali kabisa kwamba tuna jukumu la kupaendeleza mahali hapa, pawe mahali ambapo watoto wetu na wajukuu wetu watasoma kwa raha. Natumaini kwa nguvu zetu zote tutaweza kufanikisha kuchangia harambee ya maendeleo ya KLJS katika mwaka huu ambao shule yetu inaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

Baadhi ya wanafunzi tuliowahi kupita hapa tunapatikana kwenye page ya Facebook inaitwa KILUJUSE tafadhali ingia humu na toa mchango wako wa mawazo. Kamati ya alumni ya KILUJUSE inaandaa tarehe ya kikao cha pamoja, tafadhalini sana kwa wale wote ambao tupo hapa mjini tuguswe kufika siku hiyo. Na kwa wale walioko nje ya nchi na nje ya mkoa tutawaeleza ni jinsi gani mtaweza kuchangia katika tukio hili la kihistoria. 

Mungu awabariki sana na awaongezee maradufu pale mtakapotoa.

Karibu KILUJUSE - some of greatest people in this country originates here

early volunteers teams, our friends in Christ who helped us build our school

KILUJUSE pioneers

Nathan and other former students



some of the early students


Ngowo, Ezra, Khamsin Babu na Mr Adam, na huyo mzungu ni pastor  Wolf? not sure msaada jamani

Anna Mgelwa na classmates, enzi hizo wakiwa njuka - hii ilikua siku ya Pamba na wali bila shaka

Mwanzo mgumu jamani, KILUJUSE ilitokea hapa, hata sasa Mungu anatusaidia kwakweli

Library, KILUJUSE. Asante Mungu, Washaika wa KKT tanzania na marafiki zetu wa ELCA na Ujerumani. Mungu awabariki sana na awaongezee pale mlipotoa

Mama Margareth Bulugu na Wanafunzi wa miaka ya mwanzoni kabisa. Mungu akubariki mama na Tunakuombea Afya yako itengemae